Wednesday, March 20, 2013

NJAMA

SURA YA TISA

MAPAMBANO NA VIBARAKA

III

"Ohuu. Bosi umetokea wapi?". Linda aliuliza huku akitoa pumzi ndefu ya kuonyesha wasi wasi aliokuwa nao umemtoka.

"Nimetoka mahabusu".

"Pole sana bosi".

"Usinipe pole sasa hivi, mapambano bado kabisa yanaendelea, utanipa pole nikiweza kumaliza mapambano haya kwa usalama. Eddy yuko wapi?".

"Yuko katika shughuli za kujaribu kukutafuta apate kujua uliko. Lakini kila baada ya muda mchache anauliza hapa".

"Akipiga tena simu mwambie arudi haraka. Je Sherriff yuko wapi?".

"Wote wako pamoja".

"Haya kaniletee Sandwich za nyama ya kuku na niwekee glasi ya whiski ofisini kwangu. ninakwenda kunawa kidogo".

Baada ya kumaliza kunawa niliingia ofisini kwangu na kuanza kunywa whiski na Sandwich alizokuwa ameleta Linda.

"Chifu yuko?", niliuliza.

"Amesema muonane saa moja bila kukosa", Linda alijibu.

Mara simu ililia ofisini kwa Linda. Linda akashika simu yangu iliyokuwa imeunganishwa na yake. Alibonyeza kidude kimoja baada ya kuinua mkono wa simu.

"Hello nani hapo?", Linda aliuliza".

"Oh Eddy, rudi hapa haraka Bosi yuko hapa. Yuko hai kabisa ameketi kwenye kiti chake anakunywa whiski"....

"Haya asanhte", Linda aliweka simu huku akicheka.

"Nakwambia bosi ungesikia sauti ya Eddy niliposema uko hapa. utafikiri mtu aliyekwamwa na mwiba wa samaki".

Simu iliita tena ofisini kwa Linda na Linda akachukua simu.

"Hello nani hapo?", Linda aliuliza. "Ehe Unasemaje Issack... Eddy bado hajafika hapa, lakini atafika muda si mrefu, na kama una habari muhimu Bosi yuko hapa". "Oke, njoo haraka sana", Linda alijibu na kukata simu.

"Vijana wa Eddy aliokuwa amewasambaza, huyu Issack na mwenziwe ndio walikuwa na jukumu la kuangalia mienendo ya Sikazwe", alisema Linda.

"Ghafla mlango wa ofisi yangu ulifunguliwa, Sherriff, Eddy na Zabibu wakaingia ndani.

"Pole sana Bosi, sisi tulijua kwa uhakika kuwa utakuwa msambweni", Eddy alitoa pole.

Linda na Zabibu waliangaliana kwa jicho baya. Inaonekana Linda hakunda Zabibu kuja ofisini kwa bosi wake.

"Huyu anakuja kufanya nini, si afadhali angalikaa nyumbani, akawaachia wanaume hawa kazi hii. Mara nyingine kutembea na wanawake katika mapambano kama haya kunaweza kuleta mkosi".

"Mimi sina mkosi. Pilipili usiyokuwa inakuwashia nini?. Shughulika na mambo yako dada na mimi nitashughulika na yangu, usinijue kabisa", alijibu Zabibu kwa hasira.

"Haya basi yaacheni hayo mambo ya kitoto hapa tuko kazini. Sitaki kusikia uchafu mwingine wowote", niliwaonya.

Nilianza kuwaeleza yaliyonipata toka mwanzo mpaka mwisho. Nilipomaliza kuzungumza tu Issack akaingia.

"Ehe tupe maelezo", Eddy alimdai.

"Nitaanza toka jana usiku kwa faida ya wale ambao hawakupata habari hizo toka mwanzo. Sikazwe tulianza kumwona mnamo saa tisa za usiku akitokea barabara ya Bagamoyo. Alielekea moja kwa moja nyumbani kwake na hakutoka tena mpaka saa sita za mchana. Mnamo saa sita hivi aliondoka akaenda kula chakula cha mchana. Aliporudi mnamo saa saba hivi alikuja na lori dogo tani tatu likimfuata nyuma. Alifungua mlango na kuanza kutoa mizigo iliyofungwa kama mtu anayehama. Baada ya kujaza gari hili, liliondoka na nikamwambia Ismail alifuate. Ismail aliporudi alisema mizigo hiyo imetelemshwa kwenye bandari ndogo yaani pale ngalawa na meli ndogo ndogo zinapopakia mizigo yao.

"Yaani mizigo hiyo ilikuwa imefungwa kisafari?'.

"Ndio".

"Haya endelea".

"Kiasi cha saa tisa hivi walikuja watu wawili ndani ya gari, mmoja Mzungu mwingine mwafrika. Walikaa kama dakika tano tu wakaondoka. Nilimwambia Ismail awafuate. Walielekea barabara ya Bagamoyo, Ismail aliporudi alisema watu hawa waliingia barabara ya Kilimani na kuingia nyumba moja inayotazamana na Hosteli ya Tazara. Sikazwe hakutoka. Mnamo saa kumi na moja hivi alikuja mtu mwingine na gari akazungumza nae mlangoni. Maneno aliyosema yalionyesha kumkasirisha Sikazwe maana alimsukuma, na yule mtu haraka haraka akaingia ndani ya gari na kuondoka....

"Ismail alimfuata huyu mtu lakini mtu huyu aliingia Estiennes Hoteli na kuanza kunywa pombe, hivyo akamwacha akarudi. Wakati natoka Sikazwe alikuwa bado yuko ndani lakini nafikiri atatoka maana alichukua debe la mafuta ya petrol akajaza gari lake".

"Kazi nzuri umefanya".

"Asante", alijibu kwa furaha sana.

"Eddy nitayarishie gari, hapana Issack nitatumia gari lako mimi na wewe tutakwenda kumfuata Sikazwe, popote atakapokwenda. Sherriff Eddy na wengine mnisubiri hapa hapa nitarudi ila mjitayarishe kwa usiku wa kazi", niliwaeleza lakini niliona wanashangaa.

Kabla hawajaanza kusema mengi nilimwambia Linda. "Mwambie Chifu anisubiri kidogo nikichelewa kufika saa moja".

Nikatoka nje pamoja na Issack nikawaacha wamepigwa na butaa.

Niliangalia saa yangu ilikuwa saa kumi na mbili na dakika tano na kwa majira ya wakati huu ya Dar es Salaam giza lilikuwa limeingia. Tulipofika kwa Sikazwe tu tulimwona naye anafungua mlango wa gari akaweka mkoba wake ndani, kisha akaingia na kuwasha gari moto. Sisi tuliegesha gari letu kama watu wanaopunga hewa pwani saa za jioni kwani vile vile kulikuwa na magari mengine. Alipoondoka tu Sikazwe sisi taratibu tulimfuata.

Mimi ninapomfuata mtu hata awe na ujuzi wa namna gani hawezi kunitambua. Sikazwe alituongoza mpaka kwenye nyumba hii ambayo Issack alisema ilikuwa karibu na Hosteli ya tazara. Alipiga honi mbele ya lango kubwa. Tukaona askari anakuja kumfungulia akaingia ndani. Majibwa mawili makubwa yaliandamana na askari huyu. Sisi tulienda na kuegesha gari letu mbele ya baa ya Hosteli ya Tazara. Mtu yeyote angedhani tuko humo katika baa, tunakunywa.

"Unayo bastola yenye seilensa?", nilimwuliza Issack.

"Ndiyo".

"Nipe. Wewe ningoje hapa lakini uwe katika tahadhari kitu chochote kikitokea njoo haraka, umenielewa.

"Hamna wasiwasi bosi".

"Kazi ninayokwenda kuifanya ni ndogo ila majibu ndio yananipa wasiwasi".

"Nakutakia kheri, bosi".

"Nafikiri nitaihitaji".

Niliondoka na kwenda kwenye nyumba ile. Mbwa walikuwa wanabweka kila gari linapopita mbele ya ile nyumba. Niliona hii itanisaidia maana hata wakibweka halitakuwa jambo la ajabu. Niliangalia wapi upepe unatoka nikaona ulikuwa unatoka mashariki kwenda magharibi, hivi nikaamua kuingia nyumba hii kutoka magharibi kuzuia mbwa wasije wakaninusa. Nyumba ilikuwa imezungushiwa ua wenye seng'eng'e zenye miba upatao urefu wa futi sita kwenda juu. Kati ya mafunzo yangu makubwa kuruka ilikuwa mojawapo. Nilikuwa naweza kuruka futi saba wakati mwingine nane. Hivyo nilirudi nyuma nikaruka juu ya seng'eng'e na kutumbukia ndani ya ua bila kishindo maana nilitanguliza mabega.

Nilikumbuka kuwa kibao nje la lango kubwa  kilikuwa kimeandikwa jina la Tony Harrison, hivi nilijua huyu ndiye mwakilishi wa Euro-Afro. Zabibu aliwahi kunieleza habari hizi. Walivyokuwa wanahusiana na Sikazwe ndicho nilikuwa nimekuja kutafuta. Kwanza ilinibidi nitoe kikwazo kimoja yaani askari mlinzi na mbwa. Nilisikia mbwa wanabweka mbele ya nyumba, hivyo nilijibanza kwenye ukuta wa upande huu wa magharibi halafu nikanyata pole pole mpaka kwenye kona ya ukuta na mbele. Nilichungulia nikaona askari mlinzi pamoja na mbwa wake wawili. Nilikohoa yule askari akastuka akaangaza huku na huko asione kitu maana mimi nilikuwa nimeganda kama kupe kwenye ukuta. Ili kuridhisha mashaka yake alikuja upande niliokuwa akifuatana na mbwa. Alikuwa na bunduki mkononi, kwa umbo lake nikajua ni 'SAR'.

Alipofika karibu kabisa na mimi niliona mbwa wanainua mikia nikajua tayari wameninusa. Nililenga bastola yangu nikawaua wale mbwa kwa kuwapiga katikati ya vichwa kwa upesi sana kwamba yule askari alishangaa kuona mbwa wanaanguka hata bila kubweka. Alipogeuka na kuniona tayari alikuwa amechelewa, nilimrukia nikamkaba kabali taratibu mpaka alipokufa bila kutoa sauti. Nilivuta mizoga ya majibwa haya na maiti ya yule askari na kuyaweka kando ya ua upande wa magharibi kwenye seng'eng'e. Nikiwa nimeridhika na hatua yangu ya kwanza. Sasa nilichukua hatua ya pili.

Nilianza kuzunguka nyumba kwa nyuma nikielekea mashariki. Sikwenda mwendo mrefu kabla sijafika mahali nilipokuwa ninapahitaji. Nilikuwa nimefika nje ya sebule na dirisha la nyumba lilikuwa wazi, na nikasikia mazungumzo ya huko ndani kama nami niko pale pale. Hivyo nilibana tena kwenye ukuta nikaanza kusikiliza mazungumzo.

"Lakini Tonny, mimi nimrjitshidi sana lakini huyu mdudu Gamba na kundi lake amewaua watu wangu wengi sana. Fikiria Shuta na Mlambo  wameuawa. Nadhani nisingejitahidi zaidi ya hapo. Lakini hata hivyo bado nina watu wa kutosha kutekeleza kazi hii. Usiku huu huu itakwisha, usiwe na shaka.

Hii ilikuwa sauti ya Sikazwe.

"Sawa Ray, lakini naona ungejitahidi zaidi ya hapo maana lazima ile meli ndogo iondoke saa tisa za usiku ili kuwahi meli yetu ya Euro-Afro Mtwara usiku wa kesho. Tayari rubani wa meli hiyo ana habari na mpango wa kutoa mizigo ndani ya meli ndogo (scooner) na kuingiza katika meli hiyo huko Mtwara haina uangalizi sana kama bandari ya Dar es Salaam", Tonny alisema.

"Vizuri mimi nitajitahidi, tayari mizigo yote imefungwa vizuri, imebaki kusafirisha tu kwenda kwenye bandari ya meli ndogo".

"Nimepata habari kuwa unangojewa kwa shangwe na wakuu wa serikali ya Afrika Kusini. Nimewaeleza mipango yote, na wao wako tayari kuzungumza na chama chako ili damu isimwagike Nchini. Wamefurahi sana kwa kazi yetu ya kuweza kuziiba silaha za hatari ambazo zingeua wananchi wa Afrika Kusini bure, kumbe mnaweza kufikia maafikiano ya kubadilisha siasa ya Serikali ya Afrika Kusini kwa mazungumzo", Tonny Harrison alieleza.

"Na mimi nimeona ni wenda wazimu kuendeleza vita dhidi ya Afrika Kusini kwa njia ya mapambano.Lakini bado chama cha PLF kitaendeleza mapambano. Chimalamo ni mtu mwenye nia ya kuuza ubaguzi wa rangi kwa mapambano na mtutu". Sikazwe alionya.

"Si wewe unajua vitu vyao vyote na namba ya askari wao na mafunzo waliyopata askari wao pamoja na silaha walizonazo.

"Ndiyo, najua kila mbinu ya jeshi lake maana mwaka jana Kamati ya Ukombozi ya OAU ilitaka kutuunganisha. Hivyo tulipewa fursa ya kuelezana kikamilifu hali ya mali ya kila Chama kwa mwenzake. Tulikuwa wote tumekubali kuungana tukaelezana siri zote za vyama vyetu. Ni wakati tu tulipokuja na maoni ya namna ya kuweza kufikia hali ya kubadili siasa ya ubaguzi bila kumwaga damu, ndipo nilipokataa tena mpango huo wa kuunganisha vyama. Nilidai kuwa siasa ya Chama cha PLF na chama changu zilikuwa na tofauti za kimsingi ambazo hatukuweza kukubaliana. Huu ulikuwa uongo lakini ulikubalika ikaonekana tuendelee hivi tulivyo ili mradi wote tuna nia moja kwa hivyo siri zote za PLF ninazo.

"Kwa hiyo siri zote za PLF unazijua na kwa sababu wewe umejiunga na serikali ya Afrika Kusini itakuwa rahisi sana kuwateketeza wapigania uhuru wa PLF wasijaribu tena. Yaani litakuwa pigo kubwa kiasi kuwa kuweza kuimarisha chama chao kianze mapambano tena, lazima itawachukua muda mrefu, na wakati huo Ray utakuwa uanatawala pamoja na wazungu huko Afrika Kusini". Sikazwe alitoa kicheko.

"Msiwe na wasiwasi mimi nitakuwa nao bega kwa bega kuleta hali nzuri katika Afrika Kusini na nitakuwa mstari wa mbele kupinga harakati za ukombozi ambazo wakati huo zitakuwa hazina maana".

"Kesho ndiyo siku kubwa kwako utakapoingia Pretoria na kuwekewa zulia jekundu", Tonny alisema kwa sauti ya kejeli.

Bila kutambua ile kejeli Sikazwe alijibu. "Ninaisubiri kwa hamu sana. Magari yale yaliyofanya kazi tayari yamebadilishwa rangi za jeshi la Tanzania. Kwa hiyo saa nne inaweza kupitia Intercontinental Motors na kuyachukua ili kubeba ile mizigo toka bohari mpaka bandari ndogo".

"Tayari Max ameisha waarifu, au siyo ?', Tonny aliuliza.

Niliinuka taratibu kumwangalia huyu Max nikamtambua; ni yule aliyetukimbia kule kwenye uwanja wa Saba Saba.

"Mara hii nitakupata", nilijisemea moyoni maana mara moja alinikumbusha Veronika.

"Ndiyo, gari ziko tayari", Max alijibu.

"Oke mimi ninakwenda kijitayarisha saa tatu unusu ndipo nitatoka nyumbani kwangu kuelekea kwenye shughuli.

"Je kuna wasiwasi wowote?", aliuliza Tonny.

"Hamna taabu, tayari watu wa Forodha wanajua tunapeleka spea za magari Mtwara na tumeisha zungumza nao vizuri hamna taabu".

"Lakini usimsahau Gamba na wenzake", Tonny alikumbusha.

"Usiwe na wasiwasi nina askari zaidi ya mia ambao wamefundishwa mafunzo ya juu hapa hapa Tanzania. Kama Gamba na wenzake wanataka kifo vema, na waje watuingilie watakiona kilichomtoa kanga manyoya shingoni".

"Oke nakutakia upakuzi mwema".

"Max, kwa sababu wewe ndiye kiongozi wa meli hii ndogo uwe macho kusije kukatokea kosa", Tonny alimwonya.

"Wewe unanijua sifanyi kosa mara mbili", alijigamba Max.

"Haya Sikazwe nafikiri saa tisa na nusu tutaonana hapa sitalala nitakusubiri".

"Usiwe na shaka", alijibu Sikazwe huku akisimama.

"Lo, nipe tiketi yangu ya ndege kabisa".

"Chukua hii hapa imelipiwa na serikali yako unakokwenda kuwa kati ya watu wakubwa watakaoongoza nchi yenye nguvu kuzidi zote katika Afrika".

Sikazwe na Max walimwaga wakafungua mlango wakatoka nje. Tonny Harrison alibaki ameketi kwenye kiti. Kwa vile nilikuwa na wasiwasi kuwa wangeshangaa kutomwona askari mlinzi na mbwa wake, nilitoka pale dirishani nikazunguka mbele. Kwa bahati nzuri hawakushughulika kumwita askari, ila Max alikwenda akafungua mlango, Sikazwe akapitisha gari langoni, halafu Max akarudisha mlango na kuingia ndani ya gari wakaondoka.

Mimi nikaona nimepata wakati mzuri wa kuzungumza na Tonny Harrison. Nilipoangalia saa yangu nikaona ni saa moja na nusu. Saa mbili zilikuwa zinatosha kumaliza shughuli zangu na Tonny Harrison kabla sijamfuata Sikazwe hapo saa tatu na nusu. Nilifungua mlango taratibu maana ulikuwa umerudishiwa tu bila kufungwa kwa ufunguo. Nikiwa na bastola mkononi niliingia sebuleni na kumkuta Tonny Harrison ameinamia meza anasoma faili.

"Habari za kazi Tonny Harrison?".

Harrison aligeuka na kujikuta anaangalia katikati ya mdomo wa mtutu wa bastola. Pale pale aligeuka sura. Kwanza ikawa ya manjano kisha ikageuka ikawa nyekundu kama mtu aliyechapwa kofi usoni. Unajua hawa wenzetu weupe akichapwa kofi muruwa uso hugeuka na kuwa mwekundu. Alitaka kutamka neno akashindwa. Niliona alikuwa hategemei kabisa maisha mwake kukutana na wakati kama huu ambao alijikuta anatazama mdomo wa kifo.

"Habari gani?. Au umekuwa bubu?".

Nilisogea taratibu huku bastola yangu ikiwa imemlenga katikati ya uso wake. Kwa kigugumizi alijibu. "Nzuri....".

"Telemka hapo kwenye meza njoo tukae hapa kwenye makochi nina mazungumzo ya maana na wewe kabla sijaondoka".

Bila kusita aliinuka kwenye kiti na kwenda kukaa kwenye kochi. Wakati wote huu mdomo wa bastola haukumwachia hata chembe ya nafasi. Nilikwenda pale mezani alipokuwa ameacha faili nikalichukua. Nilikaa upande mwingine wa makochi tukawa tunaangaliana ana kwa ana.

"Bwana Harrison natumaini tumewahi kuonana?".

"Ndiyo, nafikiri tulionana kwenye tafrija iliyoandaliwa na Lion Club Hotelini Kilimanjaro".

Nikaweka bastola yangu kwenye paja huku macho yangu yakiwa yanamwangalia kwa makini.

"Na si mara moja au mbili?".

"Nafikiri ni mara nyingi".

"Nasikitika kusema kwamba leo sikuja kwenye tafrija ila nimekuja kuzungumza nawe kwa ajili ya suala la hatari ambalo wewe unalijua vizuri zaidi.

Faili niliyoichukua kwenye meza ilikuwa imeandikwa "SIRI" halafu kichwa cha faili kiliitwa "OPERESHENI HUJUMA". Mara moja nikajua katika faili hili ndimo kulikuwa na maelezo yote ya jinsi tukio hili lilivyofanywa na hawa majahiri. Ule ulikuwa ni ushindi thabiti hivyo niliweka faili kwenye mapaja yangu.

"Sina haja ya kujitambulisha kwako kuwa sasa hivi nimekuja kukuona kama nani, kwa sababu natambua unaelewa, au sivyo".

Ndiyo".

"Bila kupoteza muda ningependa kujua, bwana Harrison, wazo la kuziiba silaha za wapigania uhuru mkiwatumia wapigania uhuru wenyewe limetoka kwa Makaburu au kwa mataifa ya Magharibi?".

"Kwanza kabla sijajibu swali lako nataka kutoa mshangao wangu kwako jinsi ambavyo umeweza kupeleleza na kugundua jambo hili ambalo lilitayarishwa kwa mbinu za hali ya juu. Mimi ningependa unieleze kwanza jinsi ulivyoweza kupeleleza mpaka kunifikia mimi kitu ambacho sikutegemea kabisa. Nafikiri baada ya hapo unaweza kunifanya unavyotaka kwani hili faili uliloshika lina kila kitu. Sina hata haya ya kukueleza mengi; yote utayakuta humo".

Mpaka sasa nilishatambua kuwa Harrison hakuwa mtu mwenye ujuzi wowote katika mambo ya kijasusi ila alikuwa ametumiwa tu kwa sababu ndiye mtu pekee ambaye angeweza kutekeleza jambo hili bila kushukiwa, na kweli kwa muda wa miezi sita alikuwa amefaulu kutotambulikana.

"Sawa, bwana Harrison. Nafikiri nitaanzia toka mwanzo ninavyofikiri ndivyo mambo yalivyokuwa mpaka kufikia hali hii.

"Mnamo miezi sita iliyopita Rais wa Chama cha wapigania uhuru kiitwacho PLF, Ndugu Cicil Chimalamo, alitembelea Urusi kwa nia ya kutafuta msaada wa kijeshi; yaani silaha kwa ajili ya mapambano yaliyokuwa yameanza dhidi ya serikali ya Afrika Kusini.

"Kwa vile Ndugu Chimalamo alikuwa na habari zote kuhusu nguvu za kijeshi za serikali ya Afrika Kusini ilizonazo alitoa maombi yake kwa serikali ya Urusi ili aweze kupatiwa msaada wa silaha za kisasa walizonazo Makaburu. Ombi hili la Ndugu Chimalamo lilikubaliwa na serikali ya Urusi na akaahidiwa kupatiwa silaha hizi katika muda wa miezi sita. Na kwamba katika muda huo silaha hizi zitakuwa zimewasili Dar es Salaam".

Akiniangalia kwa makini, nilitoa pakiti yangu ya sigara ya aina ya Tropicana, nikatoa sigara mbili, moja nikampa na nyingine nikavuta mwenyewe, kisha nikaendelea.

"Kwa kutokana na mbinu za kisasa za kijasusi za mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi habari hizi zilinaswa. Ziliponaswa habari hizi ndipo nchi za Magharibi zilipopasha habari serikali ya Makaburu tishio lililokuwa linakuja dhidi yao. Hapo ndipo serikali ya Makaburu ilipokaa chini na kufikiri nini la kufanya. Uamuzi wa Makaburu ukawa wa kufanya ujahiri huu ndilo lilikuwa tatizo. Lakini baada ya kulishughulikia suala hili ambalo nafikiri walitupiwa wakuu wa shirika la ujasusi, yaani "BOSI", walifikiria mbinu za hali ya juu na kuamua kuwa kwa kutumia mbinu hizi wangeweza kufaulu kuziteka silaha hizi kabla hazijafika mikononi mwa wapigania uhuru. Bashiri yangu ni sawa na vipi?'.

"Mpaka sasa hujakosea kitu", alijibu.

"Makaburu ni wajanja sana na wanawajua wakuu wa vyama vya wapigania uhuru vizuri sana. Hivyo waliamua kumtumia mkuu mmoja wa wapigania uhuru ambaye walikuwa wanajua kuwa hakuwa na msimamo kamili, kwa vile walimjua alikuwa hapiganii hasa ukombozi wa waafrika wanaoonewa huko Afrika Kusini bali alikuwa akipigana ili apate cheo. Ukubwa na kujaza tumbo lake ndio ilikuwa nia yake. Hivyo waliamua kumtumia bwana Ray Sikazwe wa Chama cha SANP, ambaye ndiye alipatikana na sifa hizi walizozitaka. Walipofikia hapa kilichokuwa kimebaki ni namna gani watamwingia na kuweza kumridhisha kweli akisaidiana nao katika kuhujumu vyama vingine angepata kila alichokitaka. Hapa ndipo walipohitaji msaada wa nchi za Magharibi na hapo ndipo wewe Harrison ulipoingizwa katika njama hizi".

Nilinyamaza kidogo kiasi chs kupitisha mate.

"Kampuni yenu ya Euro-Afro ni kampuni kubwa sana, na ina rasilimali nyingi katika Afrika Kusini. Inamiliki madini ya maangamizi, chromiumu na platinumu katika Afrika Kusini. Na Afrika Kusini ndiyo nchi pekee isiyo ya kikomunisti inayotoa madini haya ambayo yanahitajika sana katika viwanda vya nchi za Magharibi. Hivyo serikali ya Makaburu ilizungumza na nchi za Magharibi zizungumze na kampuni yenu ikiwa na kisingizio kuwa kama wapigania uhuru hawa wakipata silaha hizi si serikali ya makaburu tu itaangamia, bali nchi za Magharibi zilizo na rasilimali zao nchini humo nazo zitapoteza mali zao. Kwa hivyo swala hili lilikuwa muhimu kwa nchi za Magharibi kama ilivyo kwa serikali ya Makaburu.

"Kwa vile Kampuni yenu inamiliki makampuni mengi katika nchi mbalimbali za kiafrika na mojawapo ikiwa ni Tanzania, hivyo ilionekana ndiyo kampuni pekee ambayo ingeweza kusaidia katika suala hili. Hivyo wakubwa wako waliarifiwa juu ya suala hili na hatari zake kama halitaweza kushughulikiwa haraka na kwa kikamilifu. Kwani hatari hii isingekuwa kwa Afrika Kusini tu ila pia Kampuni hii ya Kibepari ingeweza kupoteza mali zake zote ikiwa wazalendo watashinda vita vya ukombozi. Kutokana na sababu hizi wakubwa zako walikubaliana na Makaburu kuwa kulikuwa na haja ya kushirikiana ili kulinda maslahi ya Makaburu na nchi za Magharibi. Hapo ndipo ulipopashwa habari namna utakavyoshughulikia suala hili. Mpaka hapo maelezo yangu ni sawa au vipi?'.

"Sijui ulijuaje?, endelea maana nashangaa sana jinsi Afrika huru ilivyoendelea katika upelelezi".

"Habari zilipokufikia pamoja na plani yote ndipo ulipomwita bwana Ray Sikazwe na kumweleza kama ulivyoelekezwa. Ndipo ulipomdanganya kuwa serikali ya Makaburu iko tayari kufanya mazungumzo na chama chake ili wafikie uhuru wa walio wengi kwa mazungumzo bila mapambano, ila kwanza atimize sharti moja. Sharti hilo ni kusaidiana kati ya majasusi wa "BOSI" ambao wataingia Tanzania kama wanachama wa chama chake na kundi lake la wapigania uhuru lililokwisha kufundishwa mbinu za vita katika kuziteka silaha za chama cha PLF ambazo zilikuwa zikitegemewa kuwasili mjini Dar es Salaam mnamo miezi sita hivi".

"Kwani unadhani Makaburu hawawezi kutafuta suluhisho la namna hii, baada ya kutambua kuwa umefika sasa wakati wa kuanza kuwachukulia waafrika kama binadamu wenzao?", Harrison aliuliza.

"Mimi najibu kuwa baso, kwani kama nia yao ingekuwa hiyo wasingetaka suluhisho na chama kimoja tu na kwa siri, wangeliutangazia ulimwengu na kuomba vyama vyote vinavyohusika na tatizo la Afrika kusini vishiriki vyote kwa ujumla bila sharti lolote, la hasha, Harrison. Hizi zilikuwa mbinu tu za kuhujumu harakati za mapambano ya chama cha PLF ambacho kinaendelea na mapambano makali dhidi ya serikali ya Makaburu".

"Sawa nafikiri umenipa msingi wa mambo kama yalivyopangwa na serikali ya Afrika Kusini ikisaidiwa na nchi za Magharibi ambao ndio sisi. Lakini tulifaulu katika kuziteka nyara silaha hizi bila tatizo, je umekuja kugundua ni nani wanahusika?, ingawaje juzi tulipata habari kuwa wewe ni mpelelezi hatari lakini hatukuamini ungeweza kugundua kitu".

"Nitakueleza sasa. Nilipoanza upelelezi wangu siku ya kwanza tu niliona mwanga kwani mlikuwa mmefanya kosa. Kosa lenyewe lilikuwa ni kumwua kiki. Nilipokuta Kiki amekufa, tulianza kuchunguza habari zake tukakuta mambo yote aliyokuwa ameeleza juu yake si kweli, hivyo tukagundua alikuwa jasusi wa Makaburu waliokuwa wamefaulu kumweka katika ofisi ya za kamati ya Ukombozi ya OAU, na ni yeye aliyeweza kufanikisha jambo hili".

"Na mlijuaje kuwa mimi na sikazwe tunahusika?".

"Kosa jingine. Sikazwe nilipomwuliza kama anamfahamu Kiki alisema aliwahi kumwona mara moja tu wakati alipofika ofisini kwake na kumpeleka kwenye kamati ya Ukombozi ya OAU ili wamsaidie kazi. Sasa tulipofahamu kuwa Kiki alikuwa na rafiki msichana aitwae Zabibu nilimtafuta.

"Nilipofika kwake wakati mmemtuma mtu wa kwenda kumwua nikamkomboa. Yeye huyu binti alinieleza kuwa Sikazwe alikuwa rafiki mpenzi wa Kiki pamoja na wewe. Hii ilidhihilisha kuwa Sikazwe alisema uongo hivyo mara moja nikaanza kumhisi kuwa yumo katika mpango huu. Nilipojua kuwa kati ya makampuni yaliyo chini ya Euro-Afro ni pamoja na Intercontinental Motors ambao ni wakala wa magari ya "Benzi" nchini hapa nikawa na uhakika kabisa wewe unahusika. Maana magari yaliyotumiwa yalikuwa maloli makubwa ya aina ya Benzi ambayo ni sawa na yanayotumiwa na jeshi letu. Na magari yote ya jeshi kwa siku ile yameweza kufahamika yalikuwa wapi. Hivyo ikaacha sababu moja tu magari yaliyobeba zile silaha yalitoka kwenye kampuni yenu ya Intercontenental Motors ya jeshi pamoja na kuyaweka namba za bandia. Juu ya mavazi ya kijeshi wapigania uhuru wengi wanayo hivyo, hilo halikuwa tatizo kwenu. Una swali jingine?".

"Nafikiri umenielewesha vya kutosha na ninakupa hongera kwani kweli wewe ni mpelelezi maarufu si Afrika tu ila Ulimwengu mzima. Maswali mengine niliyokuwa nayo nimekwishajua majibu yake baada ya kuzungumza na wewe na kuamini mimi mwenyewe kuwa wewe huwezekani".

Ghafla mlango ulifunguliwa na Issack akaingia bastola mkononi.

"Karibu Issack samahani kwa kuchelewa nilikuwa na Bwana Tonny Harrison hapa ambaye ni mwakilishi wa kampuni ya Euro-Afro ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa tukio la bandarini".

Niliangalia saa yangu nikaona ni saa mbili.

"SWali na mwisho Harrison, silaha mmezificha wapi?".

"Sikazwe ndiye anajua, na kama umeweza kufikia hapa sidhani utashindwa hatua ya mwisho".

"Haya simama twende zetu. Issack kalete gari hapo mbele ya mlango".

Issack alitoka na Harrison bila matatizo alisimama na kuangalia sebule na vitu vilivyokuwemo kwa huzuni. Alitangulia mimi nikafuata nyuma. Nilipofika mlangoni nilizima taa, nikawa na faili kwapani na bastola ikiwa imemlenga Harrison. Nilirudisha mlango na kuelekea kwenye lango.

"Askari na mbwa wangu wako wapi?", Harrison aliuliza tulipofika kwenye lango.

"Sasa hivi wako sehemu ambayo mimi na wewe hatujafika lakini siku moja tutafika".

Issack alikuwa ameegesha gari mbele ya lango, Harrison alifunga mlango wa nyuma mimi nikamfuata na kukaa naye.

"Kwa usalama wako usijaribu kitu chochote", nilimweleza huku Issack anaondoa gari.

"Mimi hata bastola sijui kuinua, watu hawa waliniahidi ulinzi mkali na kwamba ingekuwa vigumu operesheni hii kushindwa. Kumbe wameniuza. Usiwe na wasiwasi na mimi, sijui mbinu yoyote mbele ya bastola".

Nikajua wakati wake wa kusema ukweli umefika.

"Vipi bosi?", Issack aliuliza.

"Kituo cha usalama kwa watu kama hawa".

Issack kwa sababu alielewa ni kituo gani cha usalama alikwenda moja kwa moja na kupiga honi tulipofika kwenye lango. Mlinzi alikuja akafungua lango sisi wote wawili tukatoa vitambulisho vyetu. Akastuka mara moja na kuturuhusu kuingia. Nilimwongoza Harrison mpaka kwenye ofisi ya kituo hiki cha usalama.

Nilipofika nilimkuta afisa wa zamu nikatoa kitambulisho changu, naye akastuka.

"Ndio Mzee".

"Huyu mtu awekwe chini ya ulinzi mkali mpaka utakapopata maelezo tena".

Niliomba kitambulisho chake nikachukua jina, namba na cheo chake.

Alikuwa na cheo kikubwa. Kisha nilirudi ndani ya gari.

"Moja kwa moja ofisini, maana saa tatu na nusu ndipo kazi kubwa ya kukata na shoka inaanza".

ITAENDELEA  



Naibu Waziri wa Ujenzi, Bw. Gerson Lwenge (wa tatu kulia), akiwa na maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii wakiwasubiri Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, waliotemebea mradi wa ujenzi daraja la Kigamboni, Dar es Salaam jana.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kisasa la Kigamboni, Mhandisi John Msemo (aliyesimama), akitoa ufafanunuzi kuhusu ujenzi wa daraja hilo, Dar es Salaam jana

 Wabunge wa Kamati ya Miundombinu wakifuatilia maelezo ya Mhandisi Msemo kwa makini.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau akiwakaribisha Wabunge wa Kamati ya Miundombinu, walipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Peter Selukamba.

 Maendeleo ya ujenzi wa daraja la kisasa la Kigamboni.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt Ramadhan Dau (wa tatu kushoto) na Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi John Msemo (kushoto) wakiwaongoza Wabunge wa Kamati ya Miundombinu kukagua mradi wa ujenzi wa daraja hilo Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya Mafundi wanaojenga Daraja la Kigamboni, wakiendelea na ujenzi wa daraja hilo
 Dkt Ramadhan Dau (kulia) na Mhandisi John Msemo (katikati), wakimuonyesha Mwenyekiti wa Kamati ya Miondombinu, Bw. Peter Selukamba, mahali ambapo daraja hilo litapita baada ya kukamilika na kuanza kupitika.

 Mhandisi John Msemo (kushoto), akiwatembeza kwenye eneo la mradi, Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Bw. Peter Selukamba (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara TANRODS, Mhandisi Patrick Mfugale.
 Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (kulia), akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa daraja hilo kwa Wabunge wa Kamati ya Miundombinu ya Bunge ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walipotembelea mradi huo Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Dau akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa ujenzi wa daraja hilo kwa Wabunge wa Kamati ya Miundombinu jana..
Mhandisi Karim Mataka(kushoto) akiteta na Maofisa Waandamizi wa Idara ya Uhusiano ya NSSF, Juma Kintu (kulia) na Teopista Mheta.

KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA UJENZI DARAJA LA KIGAMBONI

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Bw. Gerson Lwenge (wa tatu kulia), akiwa na maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii wakiwasubiri Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, waliotemebea mradi wa ujenzi daraja la Kigamboni, Dar es Salaam jana.
 Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kisasa la Kigamboni, Mhandisi John Msemo (aliyesimama), akitoa ufafanunuzi kuhusu ujenzi wa daraja hilo, Dar es Salaam jana
 Wabunge wa Kamati ya Miundombinu wakifuatilia maelezo ya Mhandisi Msemo kwa makini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau akiwakaribisha Wabunge wa Kamati ya Miundombinu, walipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Peter Selukamba.


 Maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt Ramadhan Dau (wa tatu kushoto) na Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi John Msemo (kushoto) wakiwaongoza Wabunge wa Kamati ya Miundombinu kukagua mradi wa ujenzi wa daraja hilo Dar es Salaam jana.
Dkt Ramadhan Dau (kulia) na Mhandisi John Msemo (katikati), wakimuonyesha Mwenyekiti wa Kamati ya Miondombinu, Bw. Peter Selukamba, mahali ambapo daraja hilo litapita baada ya kukamilika na kuanza kupitika.
 Mafundi wakiendelea na ujenzi wa daraja hilo
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja hilo kutoka NSSF, Mhandisi John Msemo (kushoto), akiwatembeza Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Bw. Peter Selukamba (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Barabara TANRODS, Mhandisi Patrick Mfugale, walipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja hilo jana.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (kulia), akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa daraja hilo kwa Wabunge wa Kamati ya Miundombinu ya Bunge ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walipotembelea mradi huo Dar es Salaam jana.
 Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Dau akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa ujenzi wa daraja hilo.

Mhandisi Karim Mataka(kushoto) akiteta na Maofisa Waandamizi wa Idara ya Uhusiano ya NSSF, Juma Kintu (kulia) na Teopista Mheta.

NSSF NA KASI YA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI

Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karim Mataka (kushoto) akimweleza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dkt. Ramadhan Dau (katikati) maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo, linalojengwa kwa ushirikiano wa Serikali na NSSF, Dar es Salaam jana Wa pili kulia ni Meneja Kiongozi wa Mradi huo Mhandisi John Msemo na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu kulia.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt Ramadhan Dau na maofisa kutoka Shirika hilo, wakitembelea mradi wa ujenzi wa daraja hilo Dar es Salaam jana.
Sehemu ya daraja la muda lililojengwa kwa ajili ya kupitisha vifaa vya ujenzi wa daraja la kisasa la Kigamboni Dar es Salaam
 Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja hili Mhandisi John Msemo (kulia) wa NSSF akiwa na Bw. Abdallah Mseri wakitembelea mradi huo jana.
Vifaa vya ujenzi vikiendelea kufanya kazi kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni.
Maofisa kutoka NSSF wakijadiliana jambo eneo la mradi wa ujenzi wa daraja hilo.
 Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi John Msemo akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt Ramadhan Dau jinsi mafundi wanavyomwaga zege wakati wa ujenzi wa daraja hilo, Dar es Salaam jana.

Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja hilo, Mhandisi Karim Mataka akiwa katika mavazi ya kazi eneo la ujenzi wa daraja hilo, Dar es Salaam jana.

Saturday, March 9, 2013

NJAMA


SURA YA TISA

MAPAMBANO NA VIBARAKA

Ilikuwa saa kumi na mbili na nusu za asubuhi wakati nilipokuwa nakaribia kumaliza kunyoa ndevu. Nilikiangakia kidevu changu kwenye kioo nikaona nilikuwa sijajinyoa vizuri. Kila wakati nilipokuwa na mawazo mengi kitu kama hiki kilikuwa kinanitokea . Lakini hata hivyo nia yangu nionekane nadhifu hivyo nilichukua tena mashine ya ndevu na kuanza kujinyoa. Nilipoona mambo yanakuwa mazuri kwenye kidevu changu, nikaanza kuoga.

Nilitoka maliwatoni na kurudi chumbani nilikokuwa nimelala. Zabibu bado alikuwa hajaamka, hivyo nilivaa taratibu ili nisije nikamshtua toka usingizini. Alikuwa na sura ya mtoto mchanga isiyokuwa na maneno. Nilimwangalia huku nikivaa. Nilipomaliza kuvaa na kuweka kila kitu changu tayari, nilikwenda nikambusu Zabibu usingizini nikaondoka ndani ya chumba na kufunga mlango taratibu.

Niliwakuta Sherriff na Eddy wamekaa sebuleni wanakunywa kahawa.

"Karibu bosi, habari za kuamka?".

"Nzuri", nilijibu, nikaa kwenye kiti cha meza ya kulia nikavuta kikombe cha chai na kujiwekea kahawa ya kutosha.

"Lazima iwe nzuri", Sherriff alijibu huku akitabasamu nikajua alikuwa na maana gani kusema hivyo.

"Usinionee wivu".

"Lazima tukuonee wivu, maana chuma kama hicho si cha kawaida.

"Bosi, vijana wameleta habari kama ulivyoomba", Eddy alisema huku akibadilisha mazungumzo.

"Ndio, wamesemaje.

"Wamesema hawakuweza kumwona Sikazwe mpaka saa tisa za usiku. Walimpata akitokea kwenye barabara ya Bagamaoyo na akielekea nyumbani kwake. Hawakuweza kujua alikuwa anatokea wapi. Na mpaka sasa hivi bado yuko nyumbani amelala. Wamenieleza kuwa ofisi za SANP hazifanyi kazi siku za Jumamosi. Na kama unavyojua leo ni Jumamosi".

"Basi waambie waendelee na wahakikishe kuwa hawapotezi hata dakika moja. Atakapoondoka nyumbani nataka kujua anaelekea wapi. Sawa?".

"Hamna taabu".

"Sasa hivi mimi ninakwenda kumwona Chifu maana nilipata habari kuwa anataka ripoti toka kwangu, maana anasumbuliwa sana na Serikali".

"Nafikiri Sherriff anaweza kuendelea kupumzika hapa, mimi nitakujulisha wakati nitakapokuhitaji".

"Sawa", alijibu Sherriff kwa mkato.

"Naomba unipatie 'machine gun' inayoweza kuchukua risasi zaidi ya mia. Niliwahi kuzitumia nilipokuwa jeshini.

"Aina gani".

"Zilizotengenezwa Urusi".

"Zipo".

"Oke niletee moja ya aina hiyo. Ikiwezekana tuma mtu aniletee mapema kusudi niishughulikie".

"Hamna taabu, utapata.

Baada ya kuzungumza na hawa vijana tuliagana kisha nikaondoka. Nilitembea kwa mguu mpaka nyumbani kwangu, ili nikabadilishe nguo. Nilifika nikafungua mlango, nikaangalia saa yangu nikaona ilikuwa yapata saa mbili kasoro robo. Nilipoingia tu ndani, roho yangu ikashtuka lakini nilikuwa nimechelewa, nilipigwa na mfuko wa mchanga kisogoni nikaanguka.

II

Nilisikia sauti ikisema ni saa tisa sasa. Sauti hiyo ndiyo ilikuwa imenizindua. Nilijikuta nimelazwa kwenye kitanda cha chuma bila godoro, na nilijikuta nimefungwa kwenye kitanda mikono na miguu. Kichwa kilikuwa kinaniuma sana, na kwa chati nilifunua nilikuta nimo kwenye chumba kidogo cha giza tupu.

Nikatuliza mawazo nikaanza kufikiri nini kimetokea. Ndipo nikatambua kuwa nilipokuwa nakwenda nyumbani kwangu saa mbili kasorobo nilipigwa na kitu nilichohisi ni mfuko wa mchanga nikaanguka chini. Tokea hapo mpaka sasa sikujua chochote. Hii ina maana kuwa nilizimia. Nikakumbuka yule mtu alisema ilikuwa saa tisa, hii ina maana nilikuwa nimezimia kwa zaidi ya masaa sita.

Nilifikiri jinsi akina Eddy, Sherriff, zabibu na Chifu walivyokuwa wamehangaika huu kujaribu kunitafuta. Hata mimi mwenyewe nilikuwa sijui hapa ni wapi. Ila nilikuwa nasikia kelele nyingi nje ya chumba hiki. Hivyo nilifikiri kuwa huenda ikawa ni sehemu ya viwanda. Sikujua ile sauti iliyosema sasa ni saa tisa ilitokea wapi, maana kulionekana kana kwamba hakukuwa na mtu ndani ya chumba hiki.

"Zaidi ya saa tisa sasa lazima waje kutupokea sisi twende tukapate chochote", nilisikia tena mtu anazungumza.

"Washa taa", sauti nyingine ikajibu.

Hivyo nikajua kuwa nilikuwa nalindwa na watu wawili ila sikuweza kuwaona kwa sababu ya giza. Taa ilipowashwa mimi nikajifanya kana kwamba bado nimezimia kabisa.

"Bado kazimia kabisa", alisema mmoja wao.

"Daktari alisema hawezi kuamka mpaka saa kumi na mbili au baada ya hapo", alijibu mwingine.

"Kama ni hivyo basi twende tukawaambie watupokee njaa inauma sana".

"Oke twende, zima taa".

Walifungua mlango na kuzima taa halafu wakafunga mlango na funguo wakaondoka. Mimi nilijinyanyua ili nione nimefungwa kiasi gani. Nilikuta ni mikono na miguu tu iliyofungwa kwenye kitanda cha chuma kipatacho futi tatu upana. Miguu ilifungwa kwa ustadi sana kiasi kuwa nilisikia kama damu haipiti na sehemu za nyayo zimekufa ganzi. Kwa upande wa mikono, mkono wa upande wa ukutani nilipoujaribu nikaona haukufungwa kwa ustadi sana, ule wa upande mwingine ndio ulifungwa kwa ustadi sana.

Nilinyanyua kichwa changu nikasikia kinauma sana, nikakirudisha chini. nilianza kufikiri namna gani nitajiokoa. Baada ya kufikiri sana nikaona njia pekee ni kujaribu kufungua hizi kamba kabla walinzi hawa hawajarudi. Hivyo nilionelea nijikaze. Ingawaje kichwani nilisikia maumivu makali. Kwa vile sehemu zote tokea tumbo, kifua na kichwa zilikuwa hazikufungwa, na kitanda kilikuwa cha futi tatu nilijikunja ili mdomo wangu ufikie kamba za mkono wa upande wa ukutani ambao haukuwa umefungwa sana.

Nilitulia tena nikamwomba Mungu. Niliupeleka mdomo wangu kwenye fundo la kamba walilokuwa wamenifungia. Kwa bahati mdomo wangu ulifika nikaanza kupitisha meno yangu kwenye kamba ili niweze kujua wamefungaje. Katika hii tafuta tafuta huku maumivu karibu yananitoa fahamu, niliuma ncha moja ya kamba, nikaivuta na fundo lote la kamba likafunguka na mkono wangu wa kulia ukawa huru.

Ilibidi nirudishe kichwa changu kipumzike maana maumivu yangu yangeweza kunifanya nizimie.

Nikiwa na mkono mmoja huru, nilipata tumaini na nguvu mpya. Nilichoomba sasa ni watu hawa wasije upesi. Kwa vile walikuwa wamesema daktari aliwaambia siwezi kuamka kabla ya saa kumi na mbili nilijua watadharau kuja ndani ya chumba hiki cha joto la kuweza kuua kabla haijakaribia saa kumi na mbili wakati wananitegemea kuamka. Nguvu mpya zilizoletwa na mawazo kuwa nimechelewa mambo mengi zilinifanya nisahau kabisa maumivu yangu.

Niliutumia mkono wangu wa kulia kufungua mkono wa kushoto. Nikiwa sasa nimeweza kufikia hatua hii niliingiwa na furaha nikaanza kushambulia kamba nilizofungwa miguuni. Kwa mtu mwenye ujuzi kama wangu hii haikunipa taabu na mara nikawa huru tayari kupambana na wadhalimu hawa.

Nilirudi nikajilaza nikaziweka kamba kijanja kana kwamba bado hazijafunguliwa. Nikawa katika hali ya kusubiri. Nilivyokuwa na bahati haikupita muda mrefu nikasikia funguo zinaingia ndani ya kufuri la mlango. Mara mlango ukafunguliwa na taa zikawashwa. Mimi nilijilaza vile vile na kujifanya bado nimezirai.

"Bado sana huyu, niliwaambia daktari alisema saa kumi na mbili. Angekuwa mtu wa hivi hivi asiye na mazoezi pigo lile lingemuua pale pale", nilisikia sauti ikisema.

"Sawa. Akiamka saa kumi na mbili itakuwa vizuri maana ndipo wakati wazee watakapomhitaji", sauti nyingine ilijibu.

"Haya shika funguo, mwangalie kwa makini akionyesha dalili ya kupata fahamu tupashe habari mara moja. Sisi tuko chumba kingine tukisubiri maelekezo zaidi kutoka kwa wazee.

"Haya asante, lakini naomba asiamke wakati nikiwa peke yangu. Nasikia mtu huyu ni hatari kubwa kabisa'.

"Wewe mwoga sana. Mtu aliyefungwa kiasi hiki unafikiri atafanya nini hata akiamka, labda awe na nguvu za kishetani".

"Huenda anazo".

"Kama anazo basi pole, yatakuwa matatizo yako".

Nikiwa katika kusikiliza mazungumza haya kidogo nicheke. Yule mtu mwingine alitoka, akabaki mlinzi mmoja ambaye alifunga mlango na kuzima taa, halafu akakaa kwenye kiti. Nilisubiri kama dakika kumi hivi nikaanza kukoroma. Yule mlinzi aliinuka na kuwasha taa na kunisogelea kitandani wakati mimi bado nimefumba mamcho. Kule kuhema kwake ndiko kulinifanya nijue yuko karibu.

"Wewe umeamka", aliuliza kwa wasiwasi, nilifungua macho yangu kwa chati nikaona alikuwa ameshika bastola akiwa amelenga kifuani pangu. Nilifanya mahesabu ya namna ya kumwingia mtu huyu nikapata.

"Ndiyo', nilijibu kwa unyonge.

Niliona macho yanamtoka, nikaona mtu huyu ameingiwa na woga na anaweza kunipiga risasi shauri ya woga nisipomwahi. Hivyo kama chui nilimrukia na wakati ule ule nikawa nimepiga bastola yake ikaanguka upande mwingine na nikampiga pigo la mkono la karate katikati ya kichwa akafa bila kujua nini kimemwua. Niliiendea bastola yake, nikamvua joho lake jekundu, nikalivaa, kisha nilifungua bastola nikakuta funguo na risasi za bastola hii. Nilifungua bastola nikakuta ina risasi tatu tu nayo ina uwezo wa kubeba kumi. Hivyo niliijaza risasi, kisha nikachemsha kidogo viungo vyangu tayari kwa kupambana na watu walioko chumba kingine. Kichwa kilikuwa bado kinaniuma lakini hakikuwa tishio kubwa.

Nilizima taa, nikajaribu kufikiri nilipo lakini nikaona bila kwenda nje haingenisaidia. chumba hiki kilionekana kilikuwa ni stoo ya vitu, hivyo nilihisi hapo nje kuna ofisi na nilifikiri kuwa ndicho chumba cha pili alichokuwa amezungjumzia yule mlinzi wa pili. Nilifungua mlango taratibu, niliangalia hali mara moja nikajua hizi zilikuwa sehemu za nyuma za bohari, au ofisi. Maana kulikuwa na chumba kinatazamana na stoo hii, halafu kulikuwa na vyumba vitatu mbele tena kwa upande wa kulia. Upande wa kushoto kulikuwa na mlango wa kutokea uwani.

Nilisikia watu wanazungumza kwenye chumba kilichokuwa kinaangaliana na mahabusu yangu. Nikajua ni hiki chumba alichozungumza yule mlinzi. Nilijiweka tayari kisha nikagonga. Mimi niliamini watajua ni mwenzao hivyo wangekuja bila tahadari kufungua mlango.

"Ngwishe", nilisikia sauti ikiita.

"Ndiyo", nilijibu kwa sauti nzito.

"Ameamka?".

"Bado".

"Funguo tu mlango haukufungwa", nilijibiwa.

Basi bastola yangu ikiwa tayari mkononi, nilifungua mlango na kuingia ndani. Kweli watu wote sita walikuwa wamwezunguka meza wanakula. Waliponiangalia na kunitambua mimi ni nani wengine chakula kiliwadondoka toka midomoni.

"Endeleeni kula, mbona mnaacha", niliwatania.

Mmoja wao alimkonyeza mwenziwe wakifikiri mimi sikuona kumbe hawakujua macho ya Willy yamefundishwa kuangalia kila mahali kwa wakati mmoja utafikiri kinyonga. Yule aliyekonyezwa alitoa bastola haraka sana lakini mimi nilijua anataka kufanya nini na kabla hata sijamtahadhalisha alikuwa tayari kufyatua, lakini mimi nilikuwa mwepesi zaidi nikampata. Wakati yeye alipofyatua risasi alimpiga mwenzake na kumwua. wawili tayari walikuwa wamekufa.

Pale pale wengine wote walisimama kila mtu akitoa bastola. Lakini niliwawahi watatu halafu nikaona yule wa nne macho yake yanaangalia mlango. Mara moja nikaanguka chini na risasi ikanikosa kwa nyuma ikapita na kumpiga yule wa nne na kummaliza, mimi pale pale nikajiviringisha na kumwahi yule wa nje. Lo nilikuwa nimeponea chupu chupu, maana kama nisingewahi kulala chini, vile vile ningekwenda kuonana na Veronika mpenzi wangu kama kweli watu huwa wanaonana tena huko ahera.

Nilitoka ndani ya jengo hili upesi upesi. Nilipofika nje nikaona niko kwenye mabohari ya Chang'ombe. Bohari hii ilikuwa imezungukwa na ua wa matofali. Nilivua joho jekundu nikapanda ua nikatokea katika uchochoro nikaanza kukimbia. Nilikadilia kuwa ilikuwa yapata saa kumi na moja. Nilipofika mbele ya bohari nilikuta ni mali ya Kampuni moja ya matairi ya magari iitwayo "Trans World Tyres", kwa sababu sikutaka kufanya uchunguzi zaidi kutokana na hali niliyokuwemo niliona teksi nikaipungia ikasimama na kumwamuru dereva anipeleke Independence Avenue haraka.

ITAENDELEA

Waziri Kabaka azindua michuano ya NSSF Media Cuo 2013

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (wa pili kushoto), akipiga mpira kuzindua mashindano ya NSSF Media Cup 2013, yanayodhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwenye viwanja vya Sigara, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Dkt. Ramadhan Dau wa tatu kulia.
 Kikosi kamili cha timu ya soka ya Changamoto kilichowafunga Habari Zanzibar mabao 3-0 leo
 Timu ya Mlimani TV iliyobigizwa bao 46-1
Mchezaji wa timu ya Netiboli ya NSSF. Zamaradi Nzowa (katikati), akijaribu kuwapita wachezaji wa timu ya Mlimani, wakati wa mchezo wa ufunguzi wa michuano ya NSSF Media Cup, inayodhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwenye viwanja vya Sigara, Dar es Salaam leo. NSSF ilishinda 46-1

 Kikosi cha Habari Zanzibar kilichobugizwa mabao 3-0 Uwanja wa Sigara Dar es Salaam leo.
Timu ya Netiboli ya NSSF iliyowagalagaza Mlimani TV mabao 46-1

NJAMA


SURA YA NANE

BINTI TANZANIA

III

Tulipofika nyumbani kwa Eddy ilikuwa saa tano za usiku. Tuliingia tukaa kwenye viti. Eddy akaleta vinywaji.

"Kifo cha Veronika kimeniuma sana, tokea sasa mimi nimeahidi nitakuwa bega kwa bega na wewe mpaka nione mwisho wa mambo haya", Sherriff aliniambia huku machozi yakimtoka.

"Sijui nikwambie nini Sherriff, maana hali niliyonayo mimi siwezi kuieleza. Afadhali tuiachie hapo hapo".

"Basi, mambo yote tumetengeneza. Chifu amesema mwili wa Veronika hauwezi kusafirishwa mpaka mwisho wa mambo yote ili aweze kupewa heshima zote za kijeshi. Hivyo mwili wake umetunzwa huko kwenye chumba cha maiti katika hospitali ya Muhimbili mpaka hapo tutakapojua mwisho wa mambo haya. Mwili wake utapewa uangalizi wa pekee hivyo hata tukichukua mwezi mzima utakuwa katika hali safi tu", Eddy alieleza.

"Jambo hili haliwezi kuchukua siku mbili zaidi. Nimeshapata mwanga mkubwa wa kutosha. Kuna kitu kidogo tu ambacho bado kinakosekana lakini naamini kesho haiishi bila kukupata kitu hicho", niliwaeleza. Kisha nikawaeleza jinsi nilivyokuwa ninafikiria mambo yalivyo toka mwanzo mpaka mwisho.

"Sasa ninachotafuta ni yale magari waliyapata wapi?.Nguo ni rahisi pamoja na vyeo kama nilivyowaeleza. nikishajua hilo basi jambo hili tutakuwa tumelitatua. Itabaki sasa kufanya shughuli ya mwisho ambayo ni kuzikamata hizi silaha na kuwakamata vibaraka hawa".

Wote walitingisha vichwa kuonyesha wamenielewa.

"Ray Sikazwe anakaa wapi?", nilimwuliza Zabibu.

"Anakaa Oysterbay, Kenyata Drive nyumba Nambari 1000/D.

"Oke, Eddy tokea sasa hivi weka vijana wa kumfuata Ray Sikazwe kila mahali anapokwenda. Ifikapo asubuhi nataka nataka nijue nyendo zake zote na sisi tutawasaidia tokea hapo. Tukiweza kufanya hivyo kazi itakuwa rahisi. Baada ya mambo yote yaliyotokea leo lazima akipata habari atakuwa na wasiwasi, hivyo lazima tu atafanya kitu cha kujinasa. Wote tutalala hapa maana ndiko mahali hapafahamiki.

"Tutaonana asubuhi", niliwaaga.

Nyumba ya Eddy ilikuwa na vyumba vitatu vya kulala. Kwa vile Zabibu alikuwa na huzuni nyingi na kwa vile mimi pia nilikuwa na huzuni tulionelea afadhali tukalala pamoja ili tuweze kuliwazana mioyo.

ITAENDELEA