Sunday, August 4, 2013

BURIANI JACKLINE WANNA

Ama kweli kifo kimepangwa na Mwenyezi Mungu, Nilipokea taarifa za kifo cha mpiganaji shupavu katika medani ya Habari, Jackline Wana kwa masikitiko makubwa, ilikuwa saa kumi na moja Alfajiri ya Jumatatu iliyopita ya Mwezi Julai mwaka huu, kupitia Radio Free Afrika, baada ya mtangazaji wa radio hiyo Wambura Mtani, kulitaja jina la Jackline Wanna kuwa Marehemu.

Taarifa hii ilinitatiza mno, nikalazimika kutafuta ukweli wa tukio hili, ndipo nilipopata habatri za kweli kuwa mpiganaji huyu hatuko nae katika dunia hii. Binafsi nimeguswa sana na kifo cha Jackline, ambaye tulifahamiana kupitia tasinia ya habari. Nilimfahamu Jackline nilipokuwa kwenye Msafara wa Rais wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa, wakati wa ziara ya kutembelea visiwa vya Ukerewe.

Nakumbuka Jackline wakati huo akiripoti habari zake kupitia gazeti la Majira, baada ya kurejea Dar es Salaam, nilishawishika kuandika makala zangu kwa ushirikiano na Jackline, kitendo ambacho kilimfanya afurahe sana na kuanza kunitumia makala na stori kutoka Mwanza.

Sina mengi ya kueleza, nimegushwa sana na kifo cha Jackline, PUMZIKA KWA AMANI MPIGANAJI MWENZETU, tulikupenda sana, lakini Mungu amekupenda zaidi.

Monday, May 27, 2013

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Bw. Abbas Mtemvu (kushoto), akiteta jambo na Mwenyekiti na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Vituka, Bi. Adelina Muluge, Dar es Salaam juzi, alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye Kata hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Bw. Abbas Mtemvu (kushoto), akikabidhi vifaa vya michezo kwa Madiwani, Kapteni Kenny Makinda wa Kata za Yombo Kilakala (kulia) na Edmound Kapinga wa Makangalawe kwa ajili ya mashindano ya Serikali za Mitaa, yatakayowakutanisha vijana wa jimbo la Temeke. Anayepokea jezi na mpira ni Mwenyekiti wa Kata ya Kilakala, Amiri Bakari.

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Bw. Abbas Mtemvu (kushoto), akikabidhi vifaa vya michezo kwa Madiwani, Kapteni Kenny Makinda wa Kata za Yombo Kilakala (kulia) na Edmound Kapinga wa Makangalawe kwa ajili ya mashindano ya Serikali za Mitaa, yatakayowakutanisha vijana wa jimbo la Temeke. Katikati ni Mwenyekiti wa Kata ya Kilakala, Amiri Bakari kwa niaba ya timu ya watoto wadogo.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Bw. Abbas Mtemvu (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata za Vituka na Kilakala, baada ya kuwakabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya Serikali za Mitaa yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

DUKA LA KISASA LA HAMIDU CITY LAZINDULIWA SAMORA

MKURUGENZI MKUU WA HAMIDU CITY  BW. HAMIDU HEMED MVUNGI AKIWA NJE YA DUKA LAKE LILILOZINDULIWA MTAA WA SAMORA  DAR ES SALAAM LEO
                                       
 WASICHANA WALEMBO WATAKAOTOA HUDUMA NDANI YA DUKA LA HAMIDU CITY
MGENI RASMI ALHAJ HEMED MVUNGI AKIKATA UTEPE KUZINDUA RASMI DUKA LA HAMIDU CITY, DAR ES SALAA LEO

 SHEREHE YA UZINDUZI WA DUKA HILO ZIKIWA ZIMEPAMBA MOTO HAPA ALHAJ MVUNGI AKIKATA KEKI SAMBAMBA NA UFUNGUZI WA SHAMPENI

HAPA WAKIGONGEANA GLASI BAADA YA KUPATA SHAMPENI


Tuesday, April 2, 2013

NJAMA

SURA YA KUMI

"UHURU UTALETWA KWA MTUTU TU"

III

Tulitoka kwenye kichochoro kimoja kati ya mabohari ya sehemu hii na kujikuta uso kwa uso na bohari ya intercontinental Motors. Tulikuta nje kuna malori matatu yanapakiwa kwa pamoja. Kulikuwa na watu wasiopungua ishirini, walikuwa wanapakia mizigo kwa kupeana. Tuliona gari la Sikazwe lakini yeye hakuwemo, hali hii ilitujulisha kuwa yumo ndani.

Penbeni kidogo ya magari haya kulikuwa na walinzi. Walikuwa hatua kama ishirini kutoka kwenye magari yaliyokuwa yanapakia kwa kila upande; baadhi yao walikuwa wamejibanza kwenye ukuta wa mabohari haya na mengine wote wakiwa na bunduki mkononi. Habari nzuri wote walivaa majoho mekundu na kofia. Nilihisi kuwa kulikuwa na askari wasiopungua ishirini hapa nje.

"Nafikiri wote mmeona ulinzi ulivyo. Kitu ninachotaka ni kufanya mashambulizi kimya kwanza mpaka tutakapolazimika kuwashambuliwa watu wa ndani. Kwa upande huu giza linatusaidia hivyo walinzi wa huku haitakuwa taabu kuwapata. kuna walinzi kama sita waliobana upande huu. Mimi na Isaack tutashambulia kushoto, Nyinyi Sherriff na Eddy mtashambulia upande wa kulia. Nawatakia kheri".

Tulipeana mikono kimya kimya kwani hatukujua nini kitatokea. Mimi nilikuwa wa kwanza kujitokeza kwenye michongoma na kubana kwenye huu ukuta wa bohari jingine. Kama hatua tatu kulikuwa na mlinzi anavuta sigara huku macho yake yakiwa kwenye gari. Nilimsogelea kimya kimya. Nilipokuwa karibu kabisa nilimsemesha.

"Sijui watamaliza saa ngapi kupakia, mimi najisikia kuchoka".

"Sijui hata..." Aligeuza uso kunijibu, nikamkata karate ya shingo upesi upesi na kumlaza chini. Nikamwashiria Isaack alipojitokeza nikamwona Eddy naye ananyata kwenda upande wa kulia. Nilimnyooshea kidole kimoja kumweleza mmoja tayari nimepata. Yeye akanitolea alama ya vidole ya V kuonyesha ushindi.

"Wewe Isaack simama hapa hapa uwe kama wewe ndiye mlinzi wa hapa, mpaka nitakapokuonyesha ishara nyingine".

"Sawa", alijibu.

Mlinzi mwingine alikuwa hatua kumi hivi na hakujua nini kimetokea. Kwa vile nilikuwa nimevaa kama yeye alifikiri mimi ni mwenzake hivyo nilikwenda tu kama mmoja wao mpaka nilipomfikia. 

"Vipi kuna wasiwasi wote?", nilimwuliza.

Aliinua kichwa.

"Hakuna....."

Kabla hajamaliza nilimkata karate ya katikati ya kichwa akafa palepale. Nilimwegemeza vizuri kwenye ukuta nikamwacha kama mtu aliye hai.

Nilimwunulia Isaack vidole viwili na yeye akawainulia Eddy na Sherriff ambao sasa nilikuwa siwaoni. Kumbe Eddy na Sherriff walikuwa wameenda kwa haraka zaidi, maana Isaack alinionyesha vidole vitatu kuonyesha wenzetu tayari walikuwa wameua watatu.

Hii ilinitia moyo sana. Upakiaji uliendelea bila wasiwasi. Mtu wa mwisho kwa upande huu alikuwa amebana kwenye kona kabisa ya ukuta wa bohari hii. Nilimwendea huku nikiwasha sigara. Na yeye alipoiona aliweka bunduki yake chini akatoa sigara.

"Sina moto afadhali umepita huku", aliniambia.

Mimi niliwasha kiberiti akaimana ili kuwasha sigara. Palepale nikamkata karate ya shingo. Bila hata kukoroma akakata roho. Nikamwegemeza ukutani halafu nikamfanyia ishara Isaack aje.

"Sawa wewe utasimama hapa mimi nawafuata walinzi wale watatu waliosimama mbele ya magari. Kama watashtuka mimi nitajitupa chini wewe wawahi". Halafu nikatoa funguo za gari.

"Pita hapa kichochoroni panda gari mpaka ofisini mwambie Chifu aje pamoja na Mkuu wa Polisi pamoja na askari watakaokuja kulinda na kuzihifadhi zana hizi baada ya mapambano. Umenielewa?".

"Sana. Nakutakia kheri".

Nilianza kutembea kuelekea kwa wale watu. Kabla hata sijafika nilisikia mlio wa 'SMG' kwa upande wa akina Sherriff. Nikajua mambo yameiva. Nikainua SMG yangu na kuwateketeza hawa walinzi waliokuwa mbele ya magari. Isaack hakupata hata muda wa kupiga risasi ila nilimwona anaingia uchochoroni na kupotea. Mimi niliruka juu ya gari lililokuwa karibu, nikakuta watu wanne walikuwa wanapanga masanduki ya silaha.

"Kumetokea nini?", niliwauliza.

Wote waligeuka na kuniangalia. Pale pale nikawaachia risasi za kuwaua kisha nikaruka chini. Milio ya bunduki ilifanya watu wote watoke ndani ya bohari na kusambaratika hovyo. Watu wote waliokuwa hapa juu walikuwa wamesharuka chini. Niliweka sanduku moja kama kinga nikaanza kutungua mtu mmoja mmoja na bastola yangu nyenye sailensa.

Kwa vile hawakusikia mlio kutoka sehemu yangu watu walipiga risasi zao kuelekea upande kwa upande wa akina Sherriff. Nilipoangalia juu ya lile gari jingine nilimwona sherriff ameseimama juu na kuwashambulia adui kwa namna ya ajabu.

Nilimfanyia ishara akaiona na yeye akanifanyia ishara ya kuonyesha kuwa Eddy alikuwa chini anajaribu kuingia ndani. Kuona hivyo nilimfanyia ishara kuwa na mimi nakwenda ndani hivyo atuchunge wote. Tulikuwa tumeuwa idadi kubwa ya askari waliokuwa wamebaki ni wachache tu.

Niliruka chini huku nikiachia risasi ovyo hata niliweza kufika kwenye ukuta wa bohari lao. Nilitupa SMG nikajitupa kwenye mlango na kujiviringisha mpaka ndani ya bohari na kama umeme nikarukia nyuma ya sanduku kubwa na kuanza kujaza risasi bastola yangu. Huko nje nilisikia bado Sherriff anaendelea kumimina risasi ili kuwazuia wasitoke nje.

Nilipoinuka niliona kama kumebaki watu kumi tu ndani; wengine wote tulikuwa tumewateketeza. Nilimwona Eddy anaviringisha na kuingia ndani. Wale watu walimwona na kabla hawajapiga risasi niliwahi wawili, wengine wote wakarudi kujificha nyuma ya masanduku.

Eddy aliruka mpaka nilipokuwa.

"Asante bosi umeniponya",

"Usinishukru ndio sababu tuko wote. Kwanza kazi mliyoifanya wewe na Sherriff sikuitegemea. Kazi imekuwa rahis kabisa".

"Kuna watu kama wangapi humu ndani?".

"Hawazidi kumi, na wote wako upande wa mashariki. Nafikiri wanamlinda Sikazwe na Max".

Huko nje kulikuwa kimya; Tukajua Sherriff anasubiri sasa kashi kashi kutoka kwetu.

"Sasa Eddy lazima tuwafanyie ujanja ili tuwapunguze. Mimi nitasimama juu ya hili sanduku ili niwadanganye. Walivyo wajinga walinzi wao watainuka ili wanipige risasi. Mimi nikiita tu jina kaa tayari na hii SMG yako kisha anza kumimina risasi. Mimi nitakuwa nimeisharuka kitambo, hivyo utawapata kama mchezo. Usiogopea kuwa unaweza kuniumiza ninakuhakikishia kuwa nitakuwa sipo".

"Lolote usemalo bosi", Eddy alijibu huku anatayarisha bunduki yake.

Niliinuka kama umeme juu ya sanduku nikawaona wote mara moja.

Nikaita

"Sikazwe?".

Hapo hapo kama umeme nikaruka nyuma ya sanduku jingine. Walinzi wanne wainuka ili kunitupia risasi huku wakiwa wamejitokeza hadi vifua. Eddy alimimina risasi na kuwashindilia wote risasi katikati ya vifua vyao wakafa pale pale. Nilimwonyesha Eddy vidole kuwa wamebaki watatu, kwani nilipokuwa nimeruka juu ya sanduku niliona wako watu saba.

"Gamba, nilisikia sauti ya Sikazwe anaita.

"Unasemaje?", nilimwuliza.

"Naomba tuzungumze, vita umeshinda.

"Sawa Sikazwe, lazima ujuwe kuwa ukombozi wa Afrika Kusini utaletwa kwa mtutu wa bunduki tu, si mazungumzo.

"Walinidanganya".

"Hawakukudanganya, shida yako ni kwamba wewe ni kibaraka; yaani unapenda cheo kuliko watu wako. Matokeo yake ndiyo haya. Hata Makaburu wafanye njama za namna gani, mwisho wake wazalendo watashinda.

Wakati tukijibishana na Sikazwe, Eddy alikuwa anatambaa chini kuelekea pale walipokuwa.

"Tafadhali tuzungumze?", aliomba.

"Umechelewa, maana umeshaipaka matope Afrika, hivyo tutakupeleka mbele ya wanamapinduzi wa Afrika ndio watakao kuhukumu".

"Huwezi kunichukua hai".

Kumbe wakati huu tunajibishana Max naye na askari mwingine walikuwa wamejivuta karibu kabisa na mimi. Ghafla nikahisi kuna kitu karibu nami.

"Bosi", Eddy aliita ambaye pia alikuwa amewaona.

Kusikia tu hivyo niliruka pale nilipokuwa na wakati huo nikawaona Max na yule kijana mwingine karibu kabisa na mimi wameinua bastola tayari kufyatua. Nilijiviringisha hewani namna ambayo hata wao walishangaa risasi zao zote zikanikosa, wakati ule ule nikaachia za kwangu nikawapata wote nao wakaanguka chini.

Sikazwe aliinuka akasimama juu ya sanduku akachukua bastola akataka kujipiga risasi. Bastola tatu zililia kwa wakati mmoja na kuupiga mkono wake. Kumbe Sherriff nae alikuwa amefika mlangoni na kuona kitendo alichotaka kukifanya akakizuia. Eddy nae aliona akazuia wakati na mimi niliona nikazuia asijipige risasi.

"Bado tunakutaka Sikazwe ukiwa hai ili ukajibu maswali ya wanamapinduzi na wapenda maendeleo ya Afrika", nilimwambia huku bado anashangaa jinsi risasi tatu zikitoka pande tofauti zilivyoweza kupiga kiganja chake tu.

Mara tunasikia usiku mzima umejaa kelele za milio ya magari ya polisi.

"Chifu yuko njiani", niliwaambia wenzangu ambao sasa tulikuwa tumemzunguka Sikazwe.

Lo, Bosi ile jiviringisha uliyotoa pale hewani sijaona hata ndani ya sinema", Eddy alinisifu.

"Mimi nilichoka kabisa; sasa naamini yote niliyoelewa. Nilifikiri mengine wanakuongezea", Sherriff alisema.

"Kuwa komandoo siyo mchezo", niliwajibu nikatabasamu.

Milio wa tahadhali ya magari ya polisi ulisogea kabisa.

"Ndio sababu sikumwona Isaack", Eddy alisema.

"Ndio sababu", nilijibu.

Tulisikia milango ya magari inafungwa kwa nguvu. Mara tukamwona Chifu na Mkuu wa Polisi wanaingia.

"Karibu Chifu, kazi imekwisha. Na mtu wenu huyu hapa na mwingine nafikiri tayari una habari naye. Ndani ya malori hapo nje kumejaa silaha, na zingine zimo humu. Mkienda bandari ndogo (dhow wharf) mtakuta meli ndogo iliyotayarishwa kwa  ajili ya kusafirisha silaha hizi, sisi hatuna zaidi", nilimweleza kwa niaba ya wenzangu.

"Kazi nzuri vijana, mmeokoa jina la Tanzania, na mmeitoa Afrika katika aibu", Chifu alijibu huku wakitupa mikono ya pongezi.

Mkuu wa polisi alitoa pingu akamfunga Sikazwe huku sura yake ikionyesha ukali.

Mara nikamwona Zabibu anakuja anakimbia akifuatiwa nyuma na Isaack. Niliwakonyeza Sherriff na Eddy, tukatoka pale haraka haraka tukawaacha Chifu na wenzake wanamshughulikia Sikazwe.

"Oh mpenzi Willy", Zabibu alinirukia shingoni.

"Hamna taabu wote tu wazima", nilimjibu.

"Ashukuriwe Mungu", Zabibu alijibu.

"Isaack gari liko wapi?".

"Oh Bosi, linakusubiri wewe".

"Twendeni zetu, acheni wazee hao wafanye shughuli zao sisi yetu tumemaliza", niliwaeleza wenzangu.

Sherriff, Eddy, Isaack, Zabibu na mimi tuliondoka na kwenda kwenye gari letu huku askari polisi tuliowapita wakitushangaa na kutupigia saluti. Tuliingia ndani ya gari letu, huku gari moja la polisi lenye mlio wa tahadhali limetutangulia.

"Je unajua tunakwenda wapi?", aliuliza.


"Sijui lakini nafikiri imebidi tupewe heshima ya 'VIP' Isaack alijubu.
Mara gari nyingine ya polisi ikatusindikiza kwa nyuma.

"Lo, utafikiri Marais", Sherriff alitania.

"Mara moja kwa miaka si mbaya", nilijibu.

"Mimi mnitelemshe kwa Margaret", Sherriff alisema.

"Ala, mipango imeshafanywa nini?", niliuliza.

"Oh, mwenzangu siku nyingi", Eddy alijibu.

"Sawa baba, kazi na dawa", nilijibu huku nikimbusu Zabibu.


Nilipoangalia saa yangu nikaona ilikuwa yapata saa sita kasoro robo.

Ilikuwa asubuhi ya Jumapili. Jua lilichomoza kutokea baharini huku miali yake ya asubuhi ikichukua rangi ya maji ya bahari na kuipitisha kwenye vioo vya chumba changu cha kulala. Mwanga huu ulimmulika Zabibu usoni ambaye alikuwa bado amelala. Hakika mwanga huu wa asubuhi ulimfanya azidi kupendeza. Asubuhi vile vile kulikuwa na upepo baridi uliotoka baharini na kutufikia sehemu hizi za Upanga. Kwa kifupi ilikuwa asubuhi njema ambayo sitaisahau.

Niliangalia saa yangu nikaona inapata saa moja kasoro dakika tatu. Nilinyanyuka na kufungua radio ili kusikia taarifa ya habari ya saa moja. Kunyanyuka kwangu kulimwamusha Zabibu ambaye alinitolea tabasamu la kukata na shoka. Na mimi nikamrudishia lile la pekee ambalo huwa nalitoa kwa nadra sana.

"Tusikilize taarifa ya habari", nilimwambia.

Baada ya mlio wa tindo sauti ya kike ikasema.

"Sasa ni saa moja kamili". Halafu ikafuatiwa ya kiume.

"Ifuatayo ni taarifa ya habari kutoka Radio Tanzania Dar es Salaam msomaji Godfrey Chalamila. Kwanza habari kwa ufupi. Majasusi wawili walioshiriki katika njama za kuiba silaha za chama cha PLF bandarini wamekamatwa.

Mwili wa msichana mwanamapinduzi Veronika Amadu aliyeuawa katika harakati za kufichua njama za wizi wa silaha utasafirishwa kwenda Freetown, Sierra Leone.

Serikali imetaifisha makampuni yote yaliyokuwa chini ya Kampuni la kibepari la Euro-Afro.

Habari kamili; Wapelelezi shupavu wa Afrika jana usiku waliwakamata majasusi wawili na kuuwa wengine wengi na kuzikomboa silaha na kuzikomboa silaha za chama cha PLF zilizokuwa zimetekwa na majasusi waliokuwa wakiifanyia kazi Afrika Kusini. Majasusi hawa ni Ray Sikazwe, aliyekuwa rais wa chama cha SANP na Tonny Harrison aliyekuwa mwakilishi wa kampuni ya Euro-Afro.

Serikali imetamka kuwa watu hawa watafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu kujibu mashitaka ya ujasusi na hujuma. Wakati huo huo kamati ya ukombozi ya OAU imelaani njama hizi za Makaburu na kusema kuwa lazima Makaburu wajue kuwa Afrika iko macho na haiko tayari kuchezewa. Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa chama cha PLF kitaongeza harakati za mapambano huko Afrika Kusini ambayo ndiyo njia pekee ya kuweza kupata uhuru wa walio wengi. Vile vile taarifa hiyo imesema kutakuwa na kikao cha kamati ndogo ya siasa mjini Dar es Salaam ili kutafuta njia ya kuviunganisha vyama vyote vya ukombozi vya Afrika Kusini, ili moto wa mapambano uweze kuwaka zaidi.

Mwili wa mwanamapinduzi shupavu hayati Veronika Amadu aliyeuawa katika harakati za kupambana na majasusi wa Makaburu ili kukomboa silaha zilizokuwa zimeibiwa bandarini utasafirishwa kwenda MJINI Freetown, Sierra Leon ambako ndiko kwao. Serikali imetoa ndege aina ya Boeng 737 ambayo itachukua na ujumbe wa kijeshi utakaosindikiza maiti hiyo pamoja na wanamapinduzi wengine. Imefahamika toka mjini Freetown kuwa mwanamapinduzi huyu atazikwa kwa heshima zote za kijeshi. Vyama vya wanamapinduzi na wapenda maendeleo duniani kote vimesema vitapeleka wawakilishi wao kwenye mazishi ya shujaa huyo.

Serikali imetaifisha makampuni yote yaliyokuwa chini ya kampuni ya kibepari ya Euro-Afro, kwa kile ilichokiita "Kujihusisha kwa kampuni hiyo na serikali ya Makaburu ili kupiga vita harakati za ukombozi. Hakuna fidia itakayotolewa. Na huo ndio mwisho wa taarifa ya habari".

Nilifunga radio baada ya taarifa ya habari maana ilinikumbusha Veronika.

"Utakwenda kwenye mazishi?", Zabibu aliuliza.

"Ndio".

"Tutakwenda wote?".

"Hamna taabu. Mambo yatatengenezwa.

TAMATI

BILA SHAKA UMEVUTIWA NA HADITHI HII YA UPELELEZI WA WIZI WA SILAHA ZA WAPIGANIA UHURU WA AFRIKA KUSINI, KAZI HII IMEFANYWA NA HAYATI E.A. MUSIBA AKITUMIA JINA LA WILLY GAMBA KAMA MPELELEZI HATARI WA AFRIKA. JIANDAE KUSOMA KITABU KIITWACHO 'UCHU'. KWA MAWASILIANO ZAIDI 0754296253, 0784296253, 0717522388.
Wananchi wa Kijiji cha Maliwanda, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara wakishiriki katika ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Stephan Wassira, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa kufanikisha kuwepo kwa shule hiyo hivi karibuni.

Tuesday, March 26, 2013

NJAMA

SURA YA KUMI

"UHURU UTALETWA KWA MTUTU TU"

Tulipoingia ofisini tulikuta wanatusubiri kwa hamu.

"Chifu anataka kukuona", Eddy alinieleza.

"Mwambie Maselina haiwezekani, nitamwona baadaye. Sasa hivi hakuna nafasi maana tukichelewa hapa mambo yote yatakuwa yameharibika. Mwambie asitoke ofisini mpaka saa sita. Asipotuona ajue basi makubwa yametupata, akituona ajue tumerudi na ushindi. Umesikia Linda?".

"Nimesikia".

"Sherriff, Eddy na Isaack mko tayari kwenda kwenye uwanja wa mapambano", niliwauliza.

"Bila wasiwasi", walijibu kwa pamoja.

"Na mimi?", Zabibu aliuliza.

"Wewe utabaki hapa na Linda. Tutaonana saa sita kama tukiwa salama.

"Mimi nataka twende wote, kama ni kufa tukafe wote"

"Kwanini unataka ukafe naye kwani yeye ni nani wako", Linda alimuuliza kwa ukali.

"Acheni upuuzi, nyinyi bakini hapa, haya mambo ya kuleteana haraha, mtatupa mkosi bure".

"Twendeni zetu", niliwaeleza wenzangu nasi tukaondoka ndani ya ofisi na kuingia ndani ya gari.

Eddy ndiye alichukua usukani na Isaack akaa naye mbele. Mimi na Sherriff tulikaa nyuma.

"Twende moja kwa moja nyumbani kwangu tukachukue silaha zaidi. Halafu tutapita nyumbani kwa Eddy kuchukua silaha tulizoacha kule. Tuna saa moja ya kujitayarisha kabla ya kuingia kwenye uwanja wa mapambano.

"Itabidi tutoke kwa Eddy mnamo saa tatu na nusu. Hii itatupa nafasi ya kuwa nje ya nyumba ya Sikazwe saa tatu na nusu. Maana ndipo yeye ataondoka kuelekea huko walikoziweka silaha".

"Kisha niliwaeleza mazungumzo yote niliyoyasikia kati ya Harrison, Sikazwe na Max.

Kwa hiyo tutakuwa watu wanne tukikabiriana na zaidi ya watu mia", Isaack alisema kwa mshangao.

"Ndiyo sababu watu kama sisi tunaitwa ni hatari. Siku moja Isaack utakapokuwa komando kama mimi utakuwa na uwezo wa kukabiliana na maadui mia peke yako. Kwa hiyo mimi naona kama ni afadhali sana kama tuko watu wanne dhidi ya watu mia. Tukitumia hamasa na maadili na moyo wa kimapinduzi sina shaka Mungu atatusaidia na tutashinda na kufichua hizi njama za Makaburu na mabeberu ya jumuia ya ulimwengu", niliwatia moyo.

"Nikiwa niko na wewe bosi, huna sina wasiwasi wowote", Eddy alisema.

"Hata mimi", Sherriff aliongeza.

"Kama ni hivyo, hata mimi ninafurahi kuwa nina jeshi lililohai na kamanda wake".

"Kutokana na ulivyoeleza komredi, watu hawa walikuwa wamepanga kuzichukua silaha hizi kwa meli ndogo kama spea ziendazo Mtwara", Sherriff alieleza.

"Sawa'.

"Baada ya kufika Mtwara wangefanya nini?", aliuliza.

"Swali zuri. Watu hawa walikuwa wamejitayarisha vizuri sana. Hili kampuni kubwa la Euro-Afro lina meli zake. Meli yake moja itakuwa inapakua mizigo Mtwara kuingia kesho. Hivyo walikuwa wamepanga kutoa silaha hizi kwenye hii meli ndogo na kuzipakia katika meli kubwa ambayo ingelikwenda kuzitelemsha Afrika Kusini...

"Mipango yote hii iko ndani ya faili nililompa Linda ampelekee Chifu. Meli hiyo ingekuwa inangojwa bandari ya East London kutelemsha zana hizi. Sikazwe angeondoka kesho kwa ndege akidai anakwenda Botswana lakini angekwenda Pretoria ambako mimi nafikiri wangemtia ndani mana nia yao haikuwa kufanya kama walivyomdanganya ila tu walitaka awasaidie kuziiba silaha kwa sababu ilikuwa rahisi kwake".

"Kwa hiyo mpaka sasa Sikazwe anakazana bure tu", Isaack alisema huku akicheka.

"Wajinga ndio waliwao", Eddy alijibu. Tulifika nyumbani kwangu, nikabadilisha mavazi kuvaa mavazi ya kikazi yaani koti na suruali yenye mifuko mingi ili kuweza kubeba silaha za kutosha.

Baada ya hapo tukaelekea kwa Eddy ambako tulijitayarisha kwa kikamilifu. Kwa bahati nzuri tulikuwa na majoho mekundu matano tuliyoyateka kwa hawa majahili. Kila mtu alichukua joho moja, maana hii ingetusaidia kuwaingilia wakidhani ni wenzao. Tulipata vile vile kofia tatu ambazo niliwagawia wenzangu. Nakwambia tulipojaribu kuvaa tulifanana na wao kabisa. Hivyo tulichoomba ni kuwa tukute bado hawajabadili mvao wao unaowatambulisha. Baada ya kuona kila kitu kimekamilika tulijiandaa kuondoka huku roho zetu zikipiga haraka haraka.

II

Ilikuwa saa tatu na dakika ishirini tulipoegesha gari yetu kando kando ya bahari huku tukiangalia nyumba ya Sikazwe. Tulimsubiri aanze safari yake hapo saa tatu na nusu. Gari lake lilikuwepo hivyo tuliamini yupo.

Saa tatu na nusu kamili kama alivyosema tuliona mlango wa mbele wa nyumba unafunguliwa Max ndiye alitoka kwanza akiwa amevalia joho jekundu na kofia. Roho yangua ilijawa na furaha. Baada ya muda kidogo Sikazwe akiwa amevaa suti nyeupe alitoka akafunga mlango, halafu wote wawili wakaingia ndani ya gari. Max ndiye aliyeingia upande wa dereva. Sikazwe akaa kwenye viti vya nyuma.

"Lo Sikazwe ameanza kupata heshima ya "VIP", Sherriff alisema na wote tukacheka.

"Yule aliyetoka kwanza alikuwa Max; anaonekana ndiye Kamanda wa jeshi hili la majahili, na haikosi ndiye aliyekwenda bandarini kama Meja Paul Liboi", niliwaeleza

"Bila shaka", alijibu Sherriff.

"Hamna taabu bosi".

Gari la Sikazwe liliondoka na kuingia Kenyatta  Drive. Tulingoja mpaka lilipofika kwenye kona ya Barabara ya Bagamoyo ndipo tukamfuata. Nakwambia mimi nikimfuata mtu hata awe na ujuzi wa namna gani hawezi kutambua. Tulifuatana moja kwa moja wakashika barabara ya Upanga, halafu wakaingia barabara ya Azikiwe kisha wakaingia Azania Front na kutokea City Drive. Muda wote huu sisi tuliwafuata taratibu.

Kisha walishika barabara inayopita kwenye ofisi za usalama barabarani nikajua wanaelekea Kurasini. Nilishangaa kwanini hawakupita Intercontinental Motors kama walivyokuwa wamepanga, lakini nilihisi wamebadilisha mipango.

Walipovuka tu ofisi za polisi wa usalama barabarani, walisimama. Mara mtu akatokea kwenye kijinjia akaja na kuzungumza nao. Mimi niliwapita kasi mpaka kwenye mzunguko wa barabara hii na barabara ya Kilwa, Nikazungukia kulia na kuingia Railway Clab na kutoka. Sisi tukawa kama tunatokea mtaa wa Gerezani. Niliendesha polepole na mara nikawaona wanatokeza kuelekea barabara ya Kilwa nasi, tukawafuata.

Tulipofika kwenye njia panda ya Kilwa na barabara iendayo kwenye ofisi za Mamlaka ya Bandari ya Tanzania wao walichukua njia iendayo kwenye ofisi za Mamlaka ya Bandri.

"Nafikiri wamezificha Shimo la Udongo", alisema Isaack.

"La hasha, mbele ya ofisi za NOTCO na UDA kuna bohari la Intercontinental Motors, kwa hiyo bila shaka ndiko wanakokwenda", alisema Eddy.

"Sawa kabisa Eddy, umenitoa usingizini, saa zote hizi nafikiria wapi wameficha silaha hizi kumbe sehemu yenyewe iki wazi kabisa", Sasa sikiwa na haja ya kuwafuata karibu karibu. Tuliwaacha wakaenda mpaka wakapotea kwani sisi tuliingia ofisi za Mamlaka ya Bandari, na tulipoona wamepotea ndipo sisi tukatoka.

Bohari ya Intercontinental Motors lilikuwa nyuma ya mabohari ya kampuni ya NOTCO. Hivyo niliegesha kwenye ofisi za NOTCO. Mlinzi wa hapa alikuja kutuuliza. Mimi niliona huyu anaweza kuleta kidamisi hivyo alipoinamisha kichwa kwenye gari nilimpiga ngumi ya uso ambayo ingemfanya alale kwa muda wa masaa kama manne hivi kabla hajapata fahamu. Kisha wote tulitelemka na kumbeba na kumpandisha kwenye lori moja lililokuwa limejaa mizigo.

"Haya mabohari ya NOTCO yana walinzi hivyo itabidi tuzunguke tutokee upande wa barabara ya Kilwa ili kuepusha rabusha kabla hatujafika maana jinsi tulivyo watu wanaweza kufikiri sisi ni majambazi", Eddy alitoa ombi.

"Hapana, sasa hivi bado mapema hata tukionana nao watafikiri ni walinzi wa usalama tu. Ili tuwe kwenye hali ya usalama zaidi lazima wote tuwafanye wakalale kwa muda". 

"Nami nilikuwa nafikiri hivyo maana wakisikia mapambano yatakapoanza wanaweza kuja kujiunga na kufa bure, au kupiga simu polisi wakaja kutuingilia kabla hatujafunga kazi sawasawa.

Hivyo rafiki zangu walinzi wote wa sehemu hii walilazwa usingizi wa masaa, sio wa NOTCO tu ila wa UDA, Shirika la Usagishaji na ofisi zote za karibu. Tulipoona kazi hii ndogo tumeimaliza tuliondoka hapo na kuelekea kwenye uwanja wa mapambano.

ITAENDELEA

Sunday, March 24, 2013

TANZANIA YAWADUWAZA MOROCCO, YAWABUGIZA 3-1 U/TAIFA

KIKOSI CHA TIMU YA TANZANIA TAIFA STARS, KILICHOWATUNGUA MOROCCO  3-1 KATIKA MCHEZO WA KUWANIA TIKETI YA KUSHIRIKI FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA NCHINI BRAZIL 2014 UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAAM LEO
STARS WAKIIMBA WIMBO WA TAIFA KABLA YA MCHEZO
 MSHAMBULIAJI WA KIMATAIFA WA TANZANIA MBWANA SAMATA (KULIA), AKICHUANA VIKALI NA MLINZI WA MOROCCO ARCHGHARIR RABARY AMBAYE BAADAE ALIPEWA KADI NYEKUNDU KWA KUTOA MANENO YA KASHFA KWA MWAMUZI HELDEL MARINS KUTOKA ANGOLA
 KIKOSI CHA TIMU YA SOKA YA MOROCCO KILICHOBUGIZWA MABAO 3-1 NA STARS
 MLINZI HODARI WA STARS SHOMARI KAPOMBE (KUSHOTO) AKIMLINDA MSHAMBULIAJI WA MOROCCO HAFIDH KARADAR 
WACHEZAJI WA STARS WAKISHANGIA BAADA YA THOMAS ULIMWENGU KUFUNGA BAO LA KWANZA DHIDI YA MOROCCO
 FURAHA YA USHINDI, STARS WAKISHANGILIA BAO LA PILI LILILOFUNGWA NA MBWANA SAMATA
 UMATI WA WATANZANIA WALIOFIKA UWANJA WA TAIFA WAKISHANGILIA BAO LA PILI
 "WAMEKWISHA", WACHEZAJI WA STARS WAKIKUMBATIANA KWA FURAHA BAADA YA KUFUNGA BAO LA TATU
 STARS WAKIOMBA DUA BAADA YA KUPATA USHINDI MNONO DHIDI YA MOROCO, JIJINI DAR ES SALAAM LEO
"KAZI MLIYOTUTUMA WATANZANIA TUMEIMALIZA". NDIVO ANAVYOSEMA KIUNGO WA STARS FRANK DUMAYO ALIYEBEBWA JUU NA THOMAS ULIMWENGU...
 MASHABIKI WA STARS WAKIONESHA BANGO LILILOTABIRI USHINDI WA MABAO 3-0 DHIDI YA MOROCCO
 KIUNGO MCHEZESHAJI WA STARS AMRI KIEMBA 9 AKIWASALIMIA MASHABIKI BAADA YA VIJANA KUMALIZA KAZI WALIYOTUMWA NA WATANZANIA