Wednesday, March 20, 2013

WAFANYAKAZI NSSF WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA NA KUTOA MISAADA

Wafanyakazi wa Kikosi Maalumu cha Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF, wakijadiliana jambo, kabla yakuwatembelea watoto yatima wa kituo cha CHAKUWAMA, Dar es Salaam jana.
 Wakibeba zawadi mbali mbali kwa ajili ya watoto yatima.
Hapa ndipo kituo cha kulelea watoto yatima kilichoko Sinza, Dar es Salaam
 Zawadi zinaendelea kutolewa na wafanyakazi wa NSSF



 Wafanyakazi wa NSSF wakimsubiri mwenyeji wao.



  Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima CHAKUWAMA, Bw. Hassan Hamis (kulia) akipokea vitabu vya maelekezo ya jinsi ya kujiunga na shirika hilo, vilivyotolewa na wafanyakazi wa NSSF jana.
 Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima CHAKUWAMA, Bw. Hassan Hamis (kulia) akiwakaribisha wafanyakazi wa NSSF, waliotembelea kituo hicho, Dar es Salaam jana.

 "Angalia simu", ndivyo anavyosema mmoja mfanyakazi wa NSSF, waliotembelea kituo cha kulelea watoto yatima Sinza, Dar es Salaam.
Mtoto yatima akiwa na wafanyakazi wa NSSF waliowatembelea jana.
Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima CHAKUWAMA, Bw. Hassan Hamis (walioshikana mikono kulia) na watoto yatima wanaolelewa katika kituo hicho wakipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa NSSF, waliotembelea kituo hicho, Dar es Salaam jana.
 Mmoja wa wafanyakazi wa NSSF akiwa na mtoto yatima wakipiga stori baada ya kuwatembelea jana kwa lengo la kuwafariji na kutoa misaada mbalimbali

 Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima CHAKUWAMA, Bw. Hassan Hamis (walioshikana mikono kulia) na watoto yatima wanaolelewa katika kituo hicho wakipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa NSSF, waliotembelea kituo hicho, Dar es Salaam jana.
"Pokea zawadi mtoto", ndivyo anavyosema mmoja wa wafanyakazi wa NSSF waliotembelea kituo cha kulelea watoto yatima CHAKUWAMA, Sinza Dar es Salaam jana


 Wafanyakazi wa NSSF wakigawa zawadi kwa watoto yatima wa Kituo cha CHAKUWAMA.
 Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima.
 Kina dada wa NSSF wakicheza mchezo wa Rede na watoto wa Kituo cha Kulalaa watoto CHAKUWAMA, walipowatembelea na kutoa misaada mbalimbali.
Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF wakionyesha zawadi mbalimbali walizowapelekea watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha CHAKUWAMA, kilichoko Sinza, Dar es Salaam
Wakicheza mpira na watoto wa kituo hicho, Dar es Salaam jana

No comments:

Post a Comment