Sunday, August 4, 2013

BURIANI JACKLINE WANNA

Ama kweli kifo kimepangwa na Mwenyezi Mungu, Nilipokea taarifa za kifo cha mpiganaji shupavu katika medani ya Habari, Jackline Wana kwa masikitiko makubwa, ilikuwa saa kumi na moja Alfajiri ya Jumatatu iliyopita ya Mwezi Julai mwaka huu, kupitia Radio Free Afrika, baada ya mtangazaji wa radio hiyo Wambura Mtani, kulitaja jina la Jackline Wanna kuwa Marehemu.

Taarifa hii ilinitatiza mno, nikalazimika kutafuta ukweli wa tukio hili, ndipo nilipopata habatri za kweli kuwa mpiganaji huyu hatuko nae katika dunia hii. Binafsi nimeguswa sana na kifo cha Jackline, ambaye tulifahamiana kupitia tasinia ya habari. Nilimfahamu Jackline nilipokuwa kwenye Msafara wa Rais wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa, wakati wa ziara ya kutembelea visiwa vya Ukerewe.

Nakumbuka Jackline wakati huo akiripoti habari zake kupitia gazeti la Majira, baada ya kurejea Dar es Salaam, nilishawishika kuandika makala zangu kwa ushirikiano na Jackline, kitendo ambacho kilimfanya afurahe sana na kuanza kunitumia makala na stori kutoka Mwanza.

Sina mengi ya kueleza, nimegushwa sana na kifo cha Jackline, PUMZIKA KWA AMANI MPIGANAJI MWENZETU, tulikupenda sana, lakini Mungu amekupenda zaidi.

No comments:

Post a Comment